Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ametoa kauli kali dhidi ya Marekani, akieleza kuwa haiwezekani kuamini taifa hilo kutokana na rekodi yake ya kuvunja mikataba na tabia ya kiburi katika mahusiano ya kimataifa.
Amesema: “Je, inawezekana kuamini Marekani na rais wake ambaye ni mvunja mikataba, mwenye kiburi na mwenye tabia ya kudhalilisha wengine? Je, tunaweza kuisahau historia yetu na kuamini Marekani?”.
Aidha, ameonya kwamba baadhi ya kauli zisizo za tahadhari kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya nchi zinaweza kuwapa maadui taswira potofu ya kuwepo kwa mgawanyiko wa ndani, jambo ambalo linaweza kutumiwa vibaya kisiasa na kisaikolojia dhidi ya Iran.
Ameongeza kuwa mshikamano wa ndani na tahadhari katika usemi wa viongozi na wananchi ni muhimu ili kuzuia adui kutumia kauli au mitazamo ya ndani kama chombo cha propaganda dhidi ya taifa.
Your Comment